Jumamosi 14 Februari 2026 - 01:30
Uakisi mpana wa maandamano ya tarehe 22 Bahman katika vyombo vya habari vya dunia

Hawza/ ushiriki wa hamasa wa wananchi wa Iran katika maandamano ya tarehe 22 Bahman, kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka arobaini na saba ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, umeibua radi amali pana katika vyombo vya habari vya kikanda na kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, tangu saa za mapema za asubuhi ya (22 Bahman), wananchi katika zaidi ya miji 1,400 na vijiji 35,000 nchini Iran walihudhuria kwa wingi na kwa mara nyingine wakaonesha uungaji mkono wao kwa malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu na uongozi wake. Zaidi ya waandishi wa habari 200 na timu za habari za kigeni zilizopo nchini Iran zilifuatilia hafla hiyo moja kwa moja kutoka uwanjani.

Al Mayadeen iliripoti katika matangazo ya moja kwa moja kutoka miji mbalimbali kwamba: Ushiriki wa wananchi wa Iran ni ujumbe wa wazi kwa maadui wa nchi hiyo kuhusu uimara wa uhusiano kati ya taifa na mfumo wa dola. Mtandao huo pia ulielezea uwepo wa Rais Masoud Pezeshkian pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wa kiraia na kijeshi.

Al Masirah TV ya Yemen ilielezea ushiriki huo wa mamilioni ya watu kuwa ni dhihirisho la umoja wa kitaifa na utayari wa kukabiliana na changamoto za kikanda, na ikaandika: Barabara za Iran ziligeuka kuwa uwanja wa kurejesha ahadi ya wananchi kwa Mapinduzi. Washiriki, wakiwa wamebeba bendera za Iran na picha za Kiongozi wa Mapinduzi, walipaza sauti kaulimbiu za kusisitiza uhuru na msimamo thabiti.

Kwa mujibu wa mitandao ya AI Ahed News ya Lebanon na Al Ahed News ya Iraq, barabara za mji mkuu na miji mingine ya Iran zilishuhudia maonesho ya silaha za ndani, zikiwemo makombora ya Fatih 110 na Haj Qasem, pamoja na mabaki ya droni za Israel zilizodunguliwa katika vita vya hivi karibuni. Mitandao hiyo ilitathmini uwepo mkubwa wa wananchi kuwa ni kielelezo cha nguvu ya kitaifa ya Iran.

Vyombo vingine vya habari kama Al Jazeera, Al Manar, Quds News Network na Alforat News pia vilitoa matangazo ya moja kwa moja ya hafla hiyo na kuiona kuwa ni ishara ya uimara wa taifa la Iran mbele ya vikwazo na mashinikizo ya kigeni.

Kwa mtazamo wa wachambuzi, matembezi ya nchini Iran hayakuwa tu sherehe ya kitaifa, bali pia yalikuwa ujumbe wa kimataifa kuhusu mwendelezo wa Mapinduzi na mshikamano wa ndani wa taifa la Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha